Blog

  • Ni ipi Tofauti kati ya UEFA Euro na UEFA NATIONS LEAGUE

    Ni ipi Tofauti kati ya UEFA Euro na UEFA NATIONS LEAGUE

    Kuna tofauti kubwa kati ya UEFA Euro na UEFA Nations League, ingawa mashindano yote mawili yanahusisha timu za taifa za Ulaya na huandaliwa na UEFA. Hizi hapa tofauti kuu:
    UEFA Euro (Ubingwa wa Ulaya)
    * Mashindano Makuu: UEFA Euro ni mashindano makuu ya soka barani Ulaya kwa timu za taifa. Ni sawa na Kombe la africa ( Afcon ) ,

    * UEFA UERO Huchezwa kila baada ya miaka minne.

    * Lengo kuu: ni kupata bingwa wa Ulaya. Hili ndilo kombe kuu la timu za taifa barani humo.

    * Timu hufuzu kucheza Euro kupitia kampeni maalum za kufuzu ambazo huchezwa kwa muda mrefu. Kama vile zinavopatikana timu za kucheza AFCON, nadhani unakumbuka mpaka Tanzania kufuzu afcon huwa zinapigwa mechi kadhaa.

    UEFA Nations League
    * Nations League ilianzishwa mwaka 2018 kwa lengo la kupunguza idadi ya mechi za kirafiki zisizo na maana na badala yake kutoa mechi zenye ushindani zaidi kwa timu za taifa.
    * Uefa Nations league Huchezwa kila baada ya miaka miwili, kwa kawaida kati ya mashindano ya Euro na Kombe la Dunia.
    * Lengo kuu: Ni Kutoa mechi zenye ushindani kwa timu za viwango tofauti, na pia kutoa njia mbadala ya kufuzu kwa Euro au Kombe la Dunia. Ina mfumo wa “ligi” (A, B, C, na D) ambapo timu hupanda ngazi au kushuka kulingana na matokeo yao.

    * Japo si mashindano makuu ulaya kama Euro,
    Nations League hutoa nafasi za ziada za kufuzu kwa Euro (kama ilivyotokea kwa EURO 2024 ambapo timu 3 zilifuzu kupitia mchujo wa Nations League) na wakati mwingine kwa Kombe la Dunia. Hivyo, matokeo katika Nations League yanaweza kusaidia timu kufuzu kwa mashindano makuu.
    * Ingawa Nations league ina kombe lake na league yenye ushindani mkubwa, lakini kombe lake halina hadhi kubwa kama Euro. Inachukuliwa zaidi kama jukwaa la kuongeza ushindani na fursa za kufuzu.

    Kwa Ufupi:
    * Euro ni mashindano makuu yanayotafuta bingwa wa Ulaya, huchezwa kila miaka minne, na timu hufuzu kupitia kampeni za kufuzu.
    * Nations League ni mashindano mapya zaidi yanayopunguza mechi za kirafiki, huchezwa kila miaka miwili, na hutoa fursa za kufuzu kwa Euro na Kombe la Dunia kupitia mfumo wake wa ligi na mchujo. That’s it nadhani umenisoma sasa, endelea kukaa karibu nasi kwa story nyingi zaidi za kimichezo hii hapa ni supa 12.

  • UNFORGATABLE SEASON FOR CHELSEA FC

    UNFORGATABLE SEASON FOR CHELSEA FC

    Moja kati ya msimu ambao klabu ya Chelsea haitowahi kuusahau basi ni msimu wa 2021-22
    ukiachana na kuwa kwenye ligi ya Uingereza epl chelsea walimaliza nafasi ya tatu.
    Lakini pia wakafanikiwa kuondoka na mataji matatu, wakishinda UEFA Super Cup na FIFA Club World Cup (kombe la Dunia la vilabu)
    Lakini ulikuwa ni moja ya msimu bora sana kwa klabu ya chelsea msimu ambao kama wangezichanga vzr basi walikuwa wanaondoka na mataji sita, eeh ndio
    Unajua Chelsea katika msimu wa 2021-22 walishiriki katika vikombe sita tofauti tofauti, 6 tournaments.
    kwanza ni
    * Premier League Epl
    * FA Cup
    * EFL Cup (Carabao Cup)
    * UEFA Champions League
    * UEFA Super Cup
    * FIFA Club World Cup
    lakini wakajikuta wanaambulia mataji matatu pekee, na kupoteza matatu
    kwenye primier league chelsea walimaliza katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya nchini Uingereza,
    Mancity wakafanikiwa kuondoka na taji hilo kwa tofauti ya alama 20.
    Uefa champions league wakaondoshwa katika hatua ya robo fainal na klabu ya real Madrid chelsea wakakutana na come back nyumbani kwao, mechi ya kwanza chelsea alishinda goli 3 kwa 2 santiago bernabeu alivorudi darajani akachezea 3 kwa 1,
    kwenye super cup wakafanikiwa kumfunga villareal katika mikwaju ya penalty baada ya kutoa sare.
    Kimbembe kikawa hapa, kwenye Fainal mbili ambazo zote walikutana na Liverpool huu msimu ulikuwa ni hatari sana Chelsea na liverpool walikutana katika fainal mbili ndani ya msimu mmoja, Fainal ya EFL Carabao Cup na FA CUP na zote Chelsea alipoteza,

    May, 14, 2022, Chelsea wakajikuta fainal ya FA CUP na mpinzani wao ni Yule yule Liverpool, katika huu mchezo yakajirudia yale yale ya fainal ya karabao Full time mechi ikamalizika kwa sare ya bila kufungana hadi kwenye extra time Nil Nil, yaani bila bila, game ikabidi imalizwe kwa mikwaju ya penalty moja. Unaukumbuka huu msimu?
    Oya zilipigwa penalty 11 katika hii mechi, zote chuma kwa Liverpool
    Sasa hii ndio ilikuwa penalty ya mwisho ya 11 kwa chelsea apo Golikipa aliyetegemewa sana na kocha Thomas tukel kocha wa chelsea kipindi hiko kuja kufanya save bwana Kepa arrizabalaga anapewa penalty ya mwisho kabisa na anapaisha na kuinyima ubingwa klabu yake ya chelsea, kilichowauma zaidi mashabiki wa chelsea ni kitendo cha kocha Thomas tukel kumfanyia sub Eduardo Mendy golikipa aliyefanya saves kibao ndani ya pitch alafu anakuja kumweka golikipa mwingine ambaye anashindwa kusave ata penalty moja
    Liverpool wakaondoka na ubingwa wa Fa Cup,

    Ikafuatia fainal ya EFL Carabao Cup, ilipigwa hii ikapigwa usiku wa Feb 27, 2022, pale Wembley Stadium jijini London, Uingereza, yakajirudia yale yale ya fainal ya FA CUP mechi ikapigwa 90 dk zikakata Chelsea 0 liverpool 0, extra time vivyo hivyo,
    Wakaenda katika mikwaju ya penalty Liverpool wakaondoka na ubingwa wakishinda Penalty 6 kwa 5,Ni msimu

    gani? mwingine unahisi ulikuwa wa moto zaidi kwa ze blues? Drop ur comment hii hapa ni supa12 ya dino television endelea kutufollow kwa taarifa nyingi zaidi za kimichezo.

  • TOP 5 BEST PENALTY I EVER SEEN

    TOP 5 BEST PENALTY I EVER SEEN

    Kuna matukio Mengi yanayotokea katika mchezo wa soka matukio ambayo, yanaacha kumbukumbu kubwa katika maisha ya watu, zinaweza kuwa kumbukumbu njema ama mbaya? Nadhani siyo kitu kigeni kushuhudia watu wakizimia, wengine wakipoteza hadi maisha yao baada ya masikitiko, ama furaha kuzidi wakati wakiangilia mchezo wa mpira miguu, katika matukio ambayo yanaweza kuwa yanaongoza kwa kuwapa heart attack, pressure na pengine kupelekea vifo kwa watu pindi wakiangalia soka basi, ni mikwaju ya Penalty, hii ndio mida pekee ambayo utawaona wale wenye pressure na roho ndogo wakigeuka nyuma, wengine kutoka kabisa katika eneo wanalotazama mpira ili tu wasishuhudie mikwaju ya penalty.
    Leo nimekusogezea Mikwaju Mitano ya Penalty iliyobeba hisia kubwa katika soka, ambayo mimi binafsi nimewahi kuishuhudia, nitaanza na namba 5 mpaka nambari 1.

    Penalty ya 5: ni penalty ya Kepa Arrizabalaga:

    Watch: Kepa fires penalty over the bar after Chelsea keeper was brought on for Carabao Cup final shootout vs Liverpool | Goal.com
    Huyu jamaa alikuwa golikipa wa chelsea na hii penalty ilikua katika mechi ya chelsea vs Liverpool,
    Ilikuwa ni fainal ya Carabao Cup kati ya Liverpool vs Chelsea mechi ilipigwa pale Wembley Stadium jijini London, Uingereza, ulikuwa ni usiku wa tarehe 27 mwezi February 2022. hii ndio fainal ya kwanza Carabao Cup Chelsea na Liverpool kukutana na fun fact msimu huo Chelsea na liverpool walikutana katika fainal mbili ndani ya msimu mmoja fainal ya Carabao cup EFL na FA cup na fainal zote zilimalizwa kwa penalty na zote liverpool walishinda,
    Sasa katika huu mchezo Full time mechi ilimalizika kwa sare ya bila kufungana hadi kwenye extra time Nil Nil, yaani bila bila, game ikabidi imalizwe kwa mikwaju ya penalty oya zilipigwa penalty 11 katika hii mechi, zote chuma kwa liverpool
    Sasa hii ndio ilikuwa penalty ya mwisho ya 11 kwa chelsea apo Golikipa aliyetegemewa sana na kocha Thomas tukel kocha wa chelsea kipindi hiko kuja kufanya save bwana Kepa arrizabalaga anapewa penalty ya mwisho kabisa na anapaisha na kuinyima ubingwa klabu yake ya chelsea, kilichowauma zaidi mashabiki wa chelsea ni kitendo cha kocha Thomas tukel kumfanyia sub Eduardo Mendy golikipa aliyefanya saves kibao ndani ya pitch alafu anakuja kumweka golikipa mwingine ambaye anashindwa kusave ata penalty moja.

    Penalty ya Nne: Ni Penalty ya Shomari kapombe beki wa klabu ya simba,

    Kapombe ala kiapo Simba | Mwanaspoti

    April 9, 2025, Shomari Kapombe anaenda kupiga penalty ya mwisho kabisa ya kuwapeleka simba sc katika nusu fainal ya Caf confederation cup katika mechi dhidi ya Almasry, baada ya simba sc kuchezea kichapo cha goli 2 kwa 0 kule nchini misri mechi ya marudiano ikapigwa Jijini Dar es Salaam Mkapa Stadium nyumbani kwa simba sc, simba wakiondoka na ushindi wa magoli 2 katika 90dk aggregateikisoma 2 kwa 2, wakaenda katika mikwaju ya penalty, Penalty zimeshapigwa tatu kwa pande zote huku camara ameshasave mbili, sasa ikafika zamu ya penalty ya Shomari Kapombe, wakati huo Macho ya mashabiki wa simba sc na watanzania wote kwaajumla yakiwa kwa kwa shomy the way, kapombe anaenda kupiga penalty hio akiwa na kumbukumbu mbaya ya miaka miwili iliyopita kumbukumbu ya kupoteza penalty ya mwisho iliyotakiwa kuwapeleka simba sc katika nusu fainal ya Caf champions league baada ya miaka 30, katika mchezo wa robo fainal dhidi ya wydad Casablanca, ni Penalty iliyojaa pressure kubwa sana si kwa kapombe tu bali hata kwa mashabiki wa klabu ya simba waliosubiri kwa takribani miaka 32 kuishuhudia simba sc ikiingia nusu fainal ya mashindano ya Caf, kwa bahati nzuri kapombe anafanikiwa kuikwamisha kambani penalty ile na Simba sc inafanikiwa kutinga nusu fainal ya Caf confederation cup.

    Penalty ya 3: ni Penalty ya Gonzalo Montiel, kwenye mchezo wa fainal ya kombe la Dunia mwaka 2022,

    Los momentos previos de Montiel al penalti que hizo Campeón a Argentina - Vamos Mi Sevilla

    mchezo ambao uliowakutanisha Argentina 🇦🇷 dhidi ya Ufaransa 🇫🇷, hii ni moja ya fainal ambayo haitawahi kusahaulika katika ulimwengu wa soka, kwanza picha linaanza mpaka dakika ya 78 Argentina wako mbele kwa magoli mawili, ndani ya dakika mbili tu dakika ya 79 na 80 kylian mbappe anabadilisha upepo kwa kusawazisha magoli yote mawili, na kwenda extra time Argentina wanaongeza goli moja Ufaransa wakarudisha klyian mbappe akiondoka na hattrik full time 3 kwa 3, wakaenda katika mikwaju ya penalty, ambapo walianza france mbappe akaweka chuma kambani, messi akaweka france wakakosa 2 argentina wakapata kolomuani akaweka upande wa france ikawa ni 3 kwa 2, hii sasa ndio ilikuwa penalty ya mwisho ambayo ilikuwa inaenda kuamua mikwaju iendelee au Argentina wakabidhiwe kombe, Gonzalo Montiel anaaminiwa na kocha kwenda kuipiga penalty mbele ya maligend penalty iliyobeba matumain mengi kwa Argentina wakiwa na kumbukumbu ya kombe lao la world cup walilolichukua
    Miaka 36 iliyopita chini ya armando maradona sasa ni utawala wa Messi, mchezaji mwenye profile ya kawaida mchezaji kutoka pale pale katika ligi ya ndani Argentina akikipiga katika klabu ya River plate, bwana Gonzalo Montiel kwanza mwamba hakuwa miongoni mwa wachezaji walionza katika mechi hio lakini Akafanikiwa kuumaliza mchezo baada ya kuizamisha kambani penalty hio na anaandika historia mpya Kwa Lionel Messi, Di maria, Rodrygo de paul, Lautaro Martinez na wengine wengi. That was Crazy 🤪.

    PENALT YA 2. Ni Didier Drogba penalty ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa champions league)

    Chelsea beat Bayern Munich in dramatic penalty shoot-out to claim the Champions League final - The Mirror

    Ilikuwa Jumamosi ya tarehe 19, May 2012: Chelsea dhidi ya Bayern Munich, kwa mara ya kwanza baada ya miaka 28, bayern munich wanapata faida ya kucheza fainal katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Arena, mchezo. Uliojaa competition kubwa sana 90 dk zikamalizika kwa sare ya goli 1-1, goli la bayern likifungwa na Tomas, La chelsea likifungwa na Didier Drogba, mechi ikaenda katika Extra time dk drogba anacheza rafu kwenye box lao na kusababisha penalty bayern wakampa jukumu robben, robben anapiga penalty hio Peter Cech akasave, extra time ikamalizika moja kwa moja, wakaenda katika mikwaju ya penalti. Didier Drogba, ambaye alikuwa amefunga bao la kusawazisha la kichwa katika dakika za mwisho za mchezo, huyo huyo Didier Drogba aliyesababisha penalty waliokosa bayern, anafunga penalti ya mwisho na ya ushindi kwa klabu ya chelsea na kwa mara ya kwanza Chelsea wanabeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya (uefa championsleague)
    Hii ni Penalty ambayo hakuna shabiki wa klabu ya chelsea atawahi kuisahau

    Penalty ya kwanza: Ni Penalty ya Asamoah Gyan,

    Asamoah Gyan's Penalty Miss 10 Years On😭

    aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya ghana, kipindi hicho asamoah akiwa ni top top player kwenye taifa la ghana, hii ni moja ya Penalty ambayo hakuna mghana wala mwafrika yeyote mpenda soka anaweza kuisahau, ni Penalty iliyojaa pressure kubwa sana, hii Penalty ilipigwa mwaka 2010 katika kombe la Dunia, kwa mara ya kwanza kabisa bara la africa linapata host wa world cup, pale kwa Madiba Africa ya kusini, na hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa ghana kufika katika hatua ya robo fainal ya kombe la Dunia, na ndio ilikuwa mara yao ya pili kushiriki world cup baada ya ile ya 2006, hii ilikuwa ni mechi dhidi ya timu ya taifa ya uruguay, kipindi cha kwanza kinatamatika ghana wakiongoza kwa goli 1, kipindi cha pili uruguay wanarudisha goli, 90 dk zinamalizika kwa sare, saa ngapi? wasiende extra time? hao mpaka extra time 120 zikamilike, pira likapigwa mpaka dakika za jioooni kabisa ghana wanapata freekick ama pigo huru karibu kidogo na box la kumi na nane ile freekick inapigwa then jamaa anaiunga kwa kichwa na ishamvuka golikipa alafu golini akiwepo mshambuliaji wa uruguay Luis Suarez, mwamba anaamua kujitwisha majukumu ya goli kipa. na kuudaka mpira, pale pale anakula Umeme, na unatengwa mkwaju wa penalty, Penalty anapewa Asamoah Gyan macho yote ya ghana na africa nzima yanamuangalia asamoah, Waganga, mashehe, wachungaji, makando wa daladala mpaka marais wa africa macho yote kwa Asamoah, Jamaa anaenda kupiga penalt hio, akaipiga kifundi kabisa lakini kwa bahati mbaya anakosa penalty ile, baada ya kugongesha mwamba, daah dk 120 zinatamatika kwa sare. wakaenda kwenye mikwaju ya penalty ghana wakatolewa na Uruguay kwa mikwaju minne kwa miwili. kumbuka kipindi hicho kama Asamoah Gyan angefunga penalty ile Ghana lingekuwa taifa la kwanza kutoka afrika kufika katika hatua ya nusu fainal ya kombe la Dunia,
    hii ni Penalty ambayo ilimfanya asamoah Gyan astafu kwa muda kuitumikia timu yake ya taifa, kila kona ya ghana, kila kona ya africa ilimuona kama jamaa kakosa penalty kimakusudi vile, kila mtu alimtupia lawama jamaa, kama maneno yangekuwa sumu basi kipindi kile jamaa tungempoteza duniani 😄

    Binafsi kwangu mimi katika maisha yangu ya ufuatiliaji wa kabumbu hii ndio
    Mikwaju mitano ya penalti ambayo nimewahi kuishuhudia mikwaju ambayo imeacha alama isiyofutika katika historia ya soka, ikionesha jinsi mchezo huu unavyoweza kuwa na mvuto na msisimko mkubwa, huku ukiwakumbusha wachezaji na mashabiki kuwa chochote kinaweza kutokea hadi filimbi ya mwisho. Je? Ni Penalty gani? Unaikumbuka zaidi kati ya hizi na je? Ni zipi Penalty zako bora za muda wote ulizowahi kuzishuhudia katika maisha yako ya soka? Drop comment yako hapo kwenye comment hii hapa ni supa12 ya dino television subscribe channel yetu ya dino television ili uwe wa kwanza kupata updates zote kutoka kwetu .

  • RODRYGO DE GOES:  THE UNDERATED PLAYER

    RODRYGO DE GOES: THE UNDERATED PLAYER

    Vitabu vya Dini husema mwenye nacho huongezewa na asiyekuwa nacho hata kile kidogo alichokuwa nacho hunyan’ganywa Si ndio?sasa kuna Muda Dunia hufanya Virse versa, kuna Muda dunia humshusha yule anayestahili kupandishwa na anayestahili kushushwa humpandisha zaidi, yaani vurugu kweli kweli mpaka unajiuliza kwani ni nini? Dunia, unamaliza hapo unajiuliza kuna uhusiano gani? kati ya ubonge na udalali kazi ngumu na sigara, boda boda na maneno mengi, ufupi na ubishi ama urefu na uzembe? hahahaha! apa ndio ujiulize kati ya mamba na kiboko nani kiboko? Ashante Shana hii ni supa12 subscribe twende sawa

    Unamfahamu Rodrygo Silva de Goes, mwamba mwenye uwezo wa maajabu, lakini chaajabu Dunia ya soka inajifanya kama haioni uwezo wake, imeamua ifunike kombe mwanetu apite.
    Daaah inasikitisha sana, Rodrygo ni moja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa kiwanjani, na anajua kulitendea haki boli sio tu brazil bali hata pale santiago bernabeu wanaujua moto wake, ni kijana mwenye rekodi nyingi za kuvutia lakini huwezi amini hazijawahi kuwavutia hata waandaaji wa ballon d’or,

    Karibu katika makala safi ya mwanasoka wa kibrazil anayekipiga Real Madrid, Rodrigo, hapa utaweza kumfahamu kiundani tutaangazia maisha yake ndani na nje ya soka.
    kabla hatujaendelea, kama bado hujasubscribe channel yetu hii ya dino television fanya kusubscribe muda huu ili uwe wa kwanza kupata updates zote kutoka kwetu,

    Jion ya jumanne ya tarehe 9, january mwaka
    2001, Katika mji wa Osasco kusini mashariki mwa sao pauli, Brazil, katika familia ya mzee Eric Batista De Goes, zilisikika kelele za kichanga akilia, kilio kilicholeta furaha kwa Denise Goes, Denise anauaga ubinti baada ya kuleta kiumbe kipya Duniani naam ni mtoto wa kiume aliyepewa jina la Rodrygo. huenda jioni ile kila mtu alitabiri yake kuhusu Rodrygo, huenda kuna waliotabiri labda atakuwa Daktari? Labda akikuwa atakuwa rubani, Lakini baba yake Eric De Goes alivyomtazama Rodrygo aliiona miguu ya mpira na aliona kipaji kikubwa cha boli ndani yake, kama ilivyokuwa kwake Eric de goes alikuwa mchezaji aliyecheza katika vilabu kadhaa brazil japo hakuwahi kufanikiwa kucheza ligi kuu wala timu ya taifa ya Brazil 🇧🇷 ila anatajwa kuwa moja ya right back mzuri kwa wakati wake.

    Rodrygo alilewa katika mazingira ya dini sana, wazazi wake ni waumini wazuri kanisani kwahiyo kanisani yalikuwa makao yake muda mwingi.

    Maisha yake ya Soka yalianzia katika akademi ya vijana ya Santos mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka kumi tu, mwanzoni rodrigo alianzia katika timu ya futsal. Rodrygo alisafiri nchi nyingi akiwa na Santos, akicheza mchezo wake pendwa wa futsal chini ya kocha mashuhuri wa futsal Barata ambaye pia aliwahi kuwa mwalimu wa Neymar, video iliyopostiwa katika YouTube rodrygo akiwa na City Futsal katika eneo la Dallas huko Texas, Marekani.
    Mnamo Julai 21, 2017, Rodrygo alisaini mkataba wake rasmi wa kwanza, akiwa na santos mkataba wa miaka mitano. Mnamo na Novemba 1 mwaka huo, akapandishwa hadi kikosi cha wakubwa.
    Novemba 4, 2017 Rodrygo aliichezea mechi yake ya kwanza ya ligi ya Série A akiwa katika kikosi cha kwanza, akiingia kama mchezaji wa akiba wa mwisho kuchukua nafasi ya Bruno Henrique katika ushindi wa nyumbani wa 3-1 dhidi ya Atlético Mineiro.
    Januari 25 iliyofuata, alifunga bao lake la kwanza la ushindi, akifunga bao la dakika za mwisho katika ushindi wa ugenini wa 2-1 wa Campeonato Paulista dhidi ya Ponte Preta.

    Rodrygo aliichezea Copa Libertadores kwa mara ya kwanza mnamo Machi 1, 2018, akichukua nafasi ya Eduardo Sasha katika kichapo cha 2-0 ugenini dhidi ya Real Garcilaso;

    akiwa na umri wa miaka 17 na siku 50, alikua mchezaji mdogo zaidi wa Santos kuonekana katika mashindano hayo. Siku kumi na tano baadaye alifunga bao lake la kwanza katika mashindano hayo, akifunga bao la pili la timu yake kupitia juhudi binafsi katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Nacional kwenye Uwanja wa Pacaembu; akiwa na umri wa miaka 17, miezi miwili na siku sita, akawa Mbrazil mdogo zaidi kufunga goli katika mashindano hayo kabla ya rekodi yake kuvunjwa na wachezaji wengine waliohitimu kutoka akademi ya vijana ya Santos, Kaiky na Ângelo.

    Rodrygo alifunga bao lake la kwanza katika ligi kuu ya kandanda ya Brazil mnamo Aprili 14, 2018, akifunga bao la mwisho katika ushindi wa nyumbani wa 2-0 dhidi ya Ceará. Mnamo Juni 3, alifunga hat-trick na pia alitoa pasi ya mwisho kwa bao la mwisho katika ushindi wa nyumbani wa 5-2 dhidi ya Vitória

    Julai 26, 2018, Rodrygo alibadilisha namba ya jezi yake kutoka 43 hadi 9 (namba ambayo tayari alikuwa ameivaa wakati wa Libertadores). Kwa msimu wa 2019, alibadilisha tena namba, sasa hadi jezi namba 11, ambayo hapo awali ilivaliwa na mchezaji mwenzake aliyehitimu kutoka akademi hio ya vijana, Neymar junior.
    Rodrygo alifanikiwa kucheza michezo 80 akiwa na Santos huku akifanikiwa kufunga magoal 17.
    Mwaka huo huo 2019 Mascout wa real madrid wakavutiwa na uchezaji wake, Don perez akazama mfukoni na kumnunua Rodrygo kwa Euro Million 45 sawa na shilling bilion 1.3 za kitanzania.

    Rodrygo akasainishwa mkataba wa miaka 6 kuitumikia real madrid toka mwaka 2019 mpaka 2025,

    Septemba 25, 2019, Rodrygo alicheza kwa mechi yake ya kwanza akiwa na real Madrid na akafanikiwa kufunga bao lake la kwanza la Laliga dhidi ya Osasuna ndani ya dakika moja tu.aliyoingia uwanjani.
    Rodrygo Alifunga hat-trick yake ya kwanza, na kutoa pasi ya bao kwa klabu hiyo Novemba 6, akiwa na umri wa miaka 18 na siku 301, dhidi ya Galatasaray katika ushindi wa 6-0 katika msimu wa Ligi ya Mabingwa ya UEFA Cl msimu 2019-20 Akiwa mchezaji wa pili mdogo zaidi kufunga hat-trick katika mashindano hayo, lakini pia akawa ni mchezaji wa kwanza aliyezaliwa katika karne ya 21 kufunga katika mashindano hayo. Katika msimu wake wa kwanza,
    Rodrygo aliweza kucheza mechi 19, huku akifunga mabao mawili wakati wa msimu wa ligi, huku Real Madrid ikishinda La Liga satander msimu. Novemba 3, 2020, Rodrygo alifunga bao la ushindi katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Inter Milan katika Ligi ya Mabingwa, UEFA Cl msimu wa 2020-21
    Aprili 12, 2022, baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA ya 2021-22 dhidi ya Chelsea, alifunga bao la dakika za jioni na kupeleka mchezo hadi dakika extra-time, ambapo Karim Benzema alifunga bao la ushindi kwa kichwa, na kuifanya Real Madrid kusonga mbele hadi nusu fainali. Aprili 30, Rodrygo akasaidia Real kutwaa taji lao la 35 la La Liga baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Espanyol kwenye uwanja wa Bernabéu. p
    Mei 4, wakiwa nyuma kwa bao 0-1 ( aggregate ikisoma 3-5) katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City, alifunga mabao mawili kati ya dakika ya 90 na 91 na kusawazisha mchezo na kuupeleka hadi dakika za ziada. Benzema alifunga penalti na kushinda mchezo kwa 3-1, na kuiruhusu Real Madrid kusonga mbele hadi fainali dhidi ya Liverpool kwa jumla ya mabao 6-5 na hatimaye wakashinda mashindano hayo.Kufuatia ushindi huo wa kusisimua dhidi ya City na michango mingine ya hivi karibuni ya ushindi wa dakika za mwisho, mchango wa Rodrygo kwa timu ulisifiwa licha ya umri wake mdogo na haraka akageuka kuwa shujaa anayeheshimika sana Madrid.

    Mnamo Aprili 18, 2023, alifunga mabao mawili katika ushindi wa ugenini wa 2-0 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA ya 2022-23, ambao ulihakikisha timu yake inafuzu kwenda nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-0. Mei 6, alifunga mabao mawili kwa Real Madrid katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Osasuna katika fainali ya Copa del Rey ya 2023, na kuwa taji lao la 20 katika mashindano hayo.
    Mnamo Novemba 2, 2023, Real Madrid ilitangaza kuufanya mabadiliko ya mkataba wa Rodrygo akasaini mkataba mpya uliongezwa ( Extended contract)ambao utamalizika Juni 30, 2028.
    Msimu huu wa 2024-2025 ukawa si msimu mzuri sana kwake alipata majeraha mara kadhaa, lakini pia klabu yake haikuwa na wakati mzuri katika mashindano yote makubwa waliyoshiriki hawakubahatika kubeba makombe
    Rodrigo amecheza mechi 42 katika mashindano yote akifanikiwa kufunga magoli 11.
    Rodrygo tangu ajiunge na real Madrid amecheza michezo 172 huku akifunga magoli 89 na assist 55.

    Rodrigo ana Laliga 2
    Uefa champions league 2
    Fifa club world cup 1
    Amechukua spanish champion cup mara 3
    Uefa super cup mara2
    fifa intercontinental cup mara 1
    spanish super cup mara 3.

    tuangazie kwa ufupi kuhusu timu yake ya taifa ya brazil
    Rodrygo aliitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha under 17, machi 30, 2017
    akaitwa kwa mara ya kwanza timu ya taifa ya wakubwa Brazil mwezi november 2019, katika Superclásico de las Américas dhidi ya Argentina ya Mess mechi ikipigwa Riyadh, Saudi Arabia. brazil wakipoteza kwa goli 1–0 on15 November.
    tangu wakati huo kila iitwapo Timu ya taifa ya brazil jina lake likawa lipo katika list,
    kwa mara ya kwanza 2022 akafanikiwa kucheza world cup akiwa na brazil
    amecheza copa america 2024. na amefanikiwa kucheza michezo 33 na kufunga goal 7.

    Nikurudishe kule mwanzo kwanini? mimi Dennis Dinomineta nabaki kuamini kuwa Rodrygo ni underated player, yaani anavochukuliwa si kama alivyo,
    Rodrygo Silva de Goes, ni kijana mwenye kipaji cha ajabu sana, nadhani miaka ijayo ukiwatafuta vijana waliokua na vipaji vya dhahabu kutoka brazil jina la Rodrygo halitawahi kukosa, rodrigo alikuwa na ndoto moja tu tangu utotoni: kuwa nyota wa soka na kushinda mataji makubwa na Real Madrid. Alifanikiwa kufikia ndoto hiyo kwa kasi ya kustaajabisha—akifunga magoli ya kusisimua Ligi ya Mabingwa, akisaidia timu yake kushinda mataji, na kuwa shujaa wa mashindano makubwa kama El Clásico na Copa América.

    Lakini, kwa kila goli alilofunga na kila mchezo aliodunda, Rodrygo alibaki kwenye kivuli cha wenzake—haswa Vinícius Júnior na Karim Benzema. Hata na uwezo wake wa kipekee wa kudribo mpira, kufunga, na kupiga pasi sahihi, mara nyingi alipewa nafasi ya kuingia kama mbadala au kucheza kwenye nafasi zisizomfaa.

    Wakati wa msimu wa 2022-23, Rodrygo alionyesha uwezo wake wa kutosha: ulikuwa ni moja ya msimu bora sana kwake, akifunga magoli 10 na assist 8 katika michezo yote ya ligi, na takwimu zake zikionyesha kuwa alikuwa miongoni mwa wachezaji bora wa Madrid wenye ubunifu na ufanisi. Lakini, licha ya mafanikio hayo, kocha Carlo Ancelotti alimweka benchi mara kwa mara, sometimes akibanwa na waandishi akimtaja Rodrygo kuwa “injury” hata wakati ambao alikuwa tayari kwa mchezo.
    kuna kipindi hadi Mashabiki walilalamikia bwana mdogo kutokupata nafasi
    Maana ilifika mahali Vini anacheza vibaya, anapoteza mpira, lakini hafanyiwi sabu afu wakati huo unakuta Rodrygo yuko benchi!

    mashabiki wakaanza kushinikiza kuwa *”Yeye ndio sababu real madrid kulishinda UCL! Kwa nini wanamsahau? bwana mdogo

    Lakini maoni ya mashabiki hayakutosha. Hata baada ya kuiokoa Madrid dhidi ya Manchester City kwa magoli mawili ya kusisimua Ligi ya Mabingwa, alibaki kuwa “mchezaji asiyepewa ile first priority.

    Mwaka huu 2025, kuna uvumi kwamba Rodrygo huenda anaweza kuondoka Madrid kwa sababu ya kukosa nafasi ya kuanza katika michezo mingi,

    watu wengi husema kuja kwa nyota kama Mbappé kunaweza kuwa kumechangia Rodrygo kutokupata nafasi na sasa anaonekana kama kivuli kwenye timu siyo mchezaji tegemezi.

    Binafsi namuona Rodrygo ni mfano wa kipaji cha dunia kilichozuiwa kuangaza kikamilifu. Ana uwezo wa kuwa kati ya wachezaji bora duniani, lakini mfumo wa timu na uamuzi wa kocha umemfanya abaki kuonekana kama “msaidizi” badala ya nyota. Daah Hadithi yake ni ya kuhuzunisha kwa sababu inaonyesha ni jinsi gani soka mara nyingi si tu kuhusu uwezo bali pia ni bahati. kuna muda unahitaji bahati kushine.

    Ukiachana na maisha yake ya soka, katika maisha yake nje ya soka Rodrygo ni kijan mpole anayependwa na watu wengi, mwaka wa jana tafiti za wachokonozi wa mambo mitandaoni walidai Rodrygo ndie mchezaji namba moja real Madrid anayewavutia zaidi watoto wakike pamoja na kupendwa na wadada wengi, lakini tayari Rodrigo ana mchumba aitwae Bruna rotta lakini pia ana watoto wawili mapacha wa kiume RAYAN na RAVY aliowapata mwaka 2022, kwa aliyekuwa mpenzi wake aitwae Pamella Cristina Costa
    Mnamo Februari 2024, Rodrygo alishirikiana na Juegaterapia na msanii Titocustoms kuzindua kampeni ya kuchangisha fedha dhidi ya saratani ya utotoni. Mpango huo, ambao ni sehemu ya kampeni ya “Kila kitu kitakuwa sawa”, ulihusisha mnada wa vitu vilivyobinafsishwa—ikiwa ni pamoja na sneakers za Nike, koti, mpira, na picha—ili kusaidia watoto walioathirika. Akizungumzia ushiriki wake, Rodrygo alisema, “Soka ni chombo kinachoturuhusu sio tu kukuza maadili ya michezo, bali pia kutoa fursa kwa watu wale wanaohitaji msaada.”
    Baba yake Rodrygo alikuwa tayari ametabiri kwamba angekuwa mchezaji wa mpira kabla hata hajazaliwa. Rodrygo ana dada mdogo mmoja, Ana Julya, aliyezaliwa mwaka 2018.

  • NEYMAR DOS SANTOS JUNIOR: Mwanamfalme aliyeshindwa kuwa mfalme

    NEYMAR DOS SANTOS JUNIOR: Mwanamfalme aliyeshindwa kuwa mfalme

    Huyu ndie aliyetabiriwa kuja kuwa mfalme baada ya ufalme wa Pele, Armando Maradona, Lionel Messi, na Cristiano Ronaldo. lakini alipangalo Mungu mwanadamu ni nani? apinge, basi huyu ndie Mwanamfalme aliyeshindwa kuwa mfalme, the prince who never become a
    king.

    Tarehe 23, ya mwezi october mwaka 1940 alizaliwa mfalme wa soka, huko nchini brazil aliyelitawala soka la Dunia kwa miongo miwili na kidogo Edson Arantes Nascimento almaarufu Pelé, mwaka 1975 Pele akiwa ameitumikia kwa miongo miwili, klabu maarufu brazil iitwayo Santos akaondoka klabuni humo na kuibukia new york cosmos alikocheza misimu miwili na kustaafu soka, tangu kipindi hicho Santos na brazil 🇧🇷 kwa ujumla haikuwa kushuhudia kipaji cha ajabu kama cha Pelé, santos ikasubiri kwa takribani miaka 8, kukishudia kipaji kingine halisi cha soka kutoka kwa Neymar da silva santos Junior.

    Karibu katika makala safi ya mwanasoka wa kibrazil aliyezaliwa na kipaji cha kipekee, kipaji halisi cha soka, hapa tutazungumzia maisha yake ya ndani ya soka, mafanikio? kufeli nk. kama bado hujasubscribe channel yetu hii ya dino television fanya kusubscribe hapo then turn on notifications twende sawa, asante.

    Neymar Da silva santos Junior, alizaliwa mwaka 1992 katika mji wa Mogi das Cruzes, jirani na sao paul huko nchini Brazil, nchi ambayo soka siyo tu kazi au burudani, bali ni utamaduni.

    Neymar Tangu utotoni, alionyesha kipaji cha ajabu. Wakati wengine wakijifunza kutembea, yeye tayari alikuwa akidunda dunda mpira Baba yake neymar bwana Neymar Santos Sr., alikitambua kipaji chake mapema na kuanza kumfundisha soka taratibu, Baba yake, Neymar Santos Sr., ambaye pia alikuwa mwanasoka wa zamani, alitambua kipawa hicho mtoto wake akiwa na umri mdogo. Neymar alitumia masaa mengi akicheza mpira katika mitaa ya kawaida ya mtaa wake, akiwa na miaka saba tu baba yake akampeleka katika akademy ya
    Portuguesa Santista, iliyokuwa karibu na kwao, Mpira ulikuwa kama sehemu ya roho yake, na mitaa ilikuwa jukwaa lake la kwanza.

    Lakini maisha hayakuwa rahisi kila wakati. Kukua katika familia ya kawaida, Neymar alikabili changamoto ambazo zingeweza kumfanya mtu mwingine kukata tamaa. Familia yake ilikumbana na shida za kifedha, na shinikizo la kufanikiwa lilikuwa kubwa. Hata hivyo, upendo wa Neymar kwa soka haukudhoofika. Alikuwa akicheza miguu mitupu kwenye uwanja wenye vumbi, ndoto zake zikiwa kubwa kuliko vizuizi alivyokabiliana nazo. Mama yake, Nadine, mara nyingi alisimulia jinsi alivyokuwa akilia kila wakati alipofikishwa ndani, akiomba dakika tano zaidi na mpira.

    Alivofika umri wa miaka 11 tu mwaka 2003, Neymar alijiunga na klabu ya santos, klabu ambayo pele alichukua ufalme wake wa soka,
    Neymar alikaa kwenye academy ya santos mpaka 2009 alivyopandishwa timu ya wakubwa neymar akiwa na miaka 17 akacheza mechi yake ya kwanza ya kimashindano akaonesha kiwango cha juu kilichomfanya kocha kumuamini na kumpa nafasi mara kwa mara akaendelea kuitumikia santos kwa mafanikio makubwa, 2011 Neymar Alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa ligi na akashinda Tuzo ya FIFA Puskás kwa jitihada binafsi kwenye ligi. Katika mwaka huohuo, aliisaidia Santos kushinda Copa Libertadores yao ya kwanza.
    kipaji cha neymar kikaendelea kukua siku hadi siku mpaka njia zake zikaanza kufanananishwa na pele,
    Pelé, ambaye mara nyingi alitajwa kama “baba” wa Neymar kwa uwezo wake wa soka, alimtazama kama mrithi wake. Lakini Neymar alikuwa na njia yake mwenyewe. Alipokuwa akikua, alishindwa kufanana na mafanikio ya Pelé, ingawa alikuwa na kipaji cha kutosha .

    2013 kipaji cha Neymar kikawaka mpaka kikaonekana Camp Nou, nyumbani kwa lionel messi, Barcelona wakazama mfukoni na kutoa kiasi cha uero million 57, sawa sawa na billion 171 za kitanzania kwa rate ya sasa, Neymar akajiunga na barcelona akamkuta mfalme wa barcelona akiendeleza utawala wake laliga, neymar akaongezeka kwenye safu ya ushambuliaji ya barca 2014 barca wakamuongeza mwamba mwingine akitokea liverpool Luis Suarez, basi ndipo ule utatu mtakatifu ukatimia utatu wa Messi, Neymar na Suarez almaarufu kama MSN kipindi hicho wapinzani wao wana BBC Bale Benzema na Cristiano, usiombe ipigwe El classicico ilikuwa balaa tupu, basi bhana neymar akaitumikia barcelona kwa mafanikio makubwa akiisaidia timu kushinda michuano mbalimbali.
    Neymar alibeba mataji mawili ya laliga, Uefa champions league moja, Copa de la rey1, Club world cup. na mengine kadhaa, pamoja na performance nzuri uwanjani Lakini majeraha yalikuwa adui wake mkubwa.

    2017 matajiri wa paris Psg wakakiona kipaji cha neymar junior, nawakaweka nia thabiti ya kumnunua wakati huo
    Barcelona ikiwa bado inamuhitaji zaidi lakini kama unavyojua pesa ni tamu kuliko asali, hakuna asiyependa kusikia habari zake, inapendwa na kila rika, kila kabila, kila taifa na kila mtu anavutiwa na kuhamasika pindi asikiapo habari za pesa basi bhana matajiri wa paris saint germain wakaweka mezani uero million 222 ambazo ni sawa na billion 666 za kitanzania kwa rate ya sasa hivi, Barcelona ni nani? Asimwachie neymar neymar akahama spain na kuingia France league 1, ambako huko alitumika Tangu 2017 hadi 2023 akiitumikia kwa mafanikio makubwa
    Neymar alichukua mataji matano 5 ya france ligue 1
    Copa de france 3
    Copa de la league 2
    Trophie de champion.

    Lakini pia alifanikiwa kucheza fainal ya uefa cl 2020 ambapo psg walipoteza mbele ya bayern munich,
    Pamoja na mafanikio hayo yote lakini bado majeraha yalikuwa yakimuandama back to back mpaka 2023 psg wakaamuuza kwa waarabu wa saudia, kwa euro million 97 sawa na billion 291 za kibongo, Neymar akaingia saudi pro league kwenye klabu ya Al hilal akasaini kandarasi ya miaka miwili huko alizioga fwedha, alikula mahela, ngwawira akawa anakula salary ya euro million 2.5 kila week yaani sawa na Bilioni 7.5 imagine ni week hio mwezi ni B 30 duuh mfano ukapewa wewe ungefanyia nini? Hela zote hizo.
    Sasa huku ndio injury zikazidi tangu alivojiunga na Al hilal hakuwai kuitumikia al hilal ata kwa nusu msimu, kwa sababu ya majeruhi ya kila mara, kuna muda alikaa muda mrefu akiuguza majeraha baadae akarudi baada ya wiki mbili tu, alivojiunge tenah na kikosi cha al hilal, katika mechi ya kwanza neyma aliingia dakika ya 57 ya mchezo akitokea benchi kwenye mechi ya Afc Champions league dhidi ya Esteghlal hakucheza dkk nyingi dkk ya 86 tu akatolewa baada ya kupata majeraha tenah, daah basi bhana msimu wa mwisho ulivomalizika Al hilal nao wakamalizana na neymar. Akabaki anasubiri dili lingine.

    Kama ilivyo kwenye maisha kuna wakati, Utakataliwa kila sehemu, kuna wakati watakuchafua kila mahali, kuna wale waliokuwa wakikukubali kisa mali, umarufu wako ama vingenevyo, wakati vikipotea watakupotea bila kujali lakini, kumbuka kuna Nyumbani, nyumbani ndio mahala pa mwisho lilipo tumaini lako ambapo kila mtu atakupokea huko, haijalishi ni nini? umepitia, haijalishi mabaya au shida kiasi gani ulizonazo lakini Nyumbani kutabaki kuwa nyumbani
    basi neymar Junior dos Santos baada ya kuona kila sehemu hatakiwi, kila klabu ikifikiria kumsajili inaona hasara maana muda wowote anaweza kupata injury na asiitumikie klabu ipasavyo, wengine wakijisemea Neymar ni mchezaji mzuri ila shida injury, hatununui vilema sisi, basi Neymar akaikumbuka ile kauli ya nyumbani ni nyumbani hata kama ni shambani, japo nabii hakubariki kwao, ila mcheza kwao hutuzwa, na sikuzote zimwi likujualo halikuli likakwisha,
    Baada ya miaka 12, mwamba akaamua kurudi nyumbani, sehemu kilipozikwa kitovu chake, katika ardhi ya Sao pauli kusini mwa Brazil, neymar akarudi katika timu yake ya utotoni mahali aliposhika mpira kwa mara ya kwanza, mahali alipojulia kupiga vyenga vya maudhi, sehemu iliyomkuza kimwili, kiroho mpaka kiakili, Santos football club, Naam wazazi wake wa football wakampokea tenah, mwanamfalme wa soka. wakamwambia kijana hapa ndipo nyumbani karibu nyumbani. basi bhana tarehe 18 February 2025 Neymar akasaini kandarasi ya miezi 6 ya kuitumikia klabu ya yake hio ya zamani, na mapokezi yake yanatajwa kuwa watu wapatao elfu 20 katika uwanja wa Belmiro walipata kuhudhuria tafrija ya kumkaribisha tenah mwana mfalme wa soka Neymar Junior dos Santos. Neymar alipopewa nafasi ya kuzungumza mbele ya umati wa mashabiki hakuwa na mengi ya kusema. Basi bhana akaendelea kukipiga santos baada ya mechi kadhaa akapata injury tenah. Mpaka sasa amecheza michezo 7 pekee akiwa na santos akifunga magoli matatu na asists tatu.

    Hebu tuangazie maisha yake ya soka la kimataifa, Neyma junior aliitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya vijana ya brazil Under 17 mwaka 2009, baada ya kutimiza miaka 18 akaitwa timu ya wakubwa kwa mara ya kwanza tokea hapo akawa anaitwa mara kwa mara

    Neymar amecheza kombe la Dunia mara 3,
    Neymar ndie Top scorer of all time ( yaani mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya brazil akiwa na magoli 79.
    2013 alishinda fifa confederation cup akiwa na brazil lakini pia
    Ana medal ya dhahabu ya Rio 2016. Katika Olympic.
    Neymar ni moja ya wachezaji wenye mafanikio mengi sana katika soka, pamoja na injury zote ila bado
    Neymar yupo kwenye orodha ya wachezaji waliowahi kufunga magoli mengi, kwenye maisha yao ya soka. Katika mechi 717 alizocheza katika maisha yake ya soka Neymar amaefunga magoli 439. Imajini isinekuwa mambo ya majeraha jamaa angukua na ballon d’or ngapi? Kabatini.

    Ama kweli, He is A prince who never became a king

    Neymar hakuwahi kuwa mfalme wa soka, lakini alikuwa na hadithi ya kipekee. Alipigana na majeraha, matarajio makubwa, na mazingira magumu, lakini alibaki kuwa mchezaji wa kuvutia na mwenye kipaji kikubwa sana.

    hayo yalikuwa ni maisha ya ndani soka ya Neymar Junior embu tuangazia kidogo maisha yake ya nje ya soka.

    Neymar si mchezaji wa soka pekee; pia ni mpenzi wa michezo ya video, yaani Video Games anacheza sana play stations, na Ana uhusiano wa karibu na ulimwengu wa eSports, na mara nyingi huonekana akicheza Fortnite au CS:GO kwenye mitandao ya twitch. Mwaka 2020, alianzisha timu yake ya eSports, Neymar Jr. Esports Team

    Mbali na kuwashangaza watu uwanjani, Neymar ni mtu wa kujitoa sana katika maswala ya kijamii.

    Mwaka 2014, alizindua shirika la Instituto Neymar Jr. huko Praia Grande, Brazil, lenye lengo la kusaidia watoto wenye mahitaji katika elimu, michezo, na fursa za kiafya. Mpango huo umesaidia zaidi ya watoto 10,500 na familia zao,
    Hata wakati ambao alipata lizikizo za majeruhi katika soka, basi mara kadhaa alionekana akiwa karibu na watoto wenye mahitaji maalumu, akionyesha upendo wake wa kina kwa watoto hao.

    Neymar ni mwanamitindo wa asili eeh, yaani ni kwamba mwamba hajawahi kusomea mitindo ila Ana sifa ya kuvutia kwenye mitindo yake mbalimbali—
    mara kadhaa utakuta ameziweka rangi nywele zake, na huziweka katika staili mbali mbali, kitu ambacho kinawavutia hadi wachezaji wanaochipukia, nyota wa sasa wa klabu ya Barcelona bwana mdogo Lamine Yamal katika moja ya mahojiano yake, aliwahi kusema anakubali style za nywele hata uchezaji wa neymar Junior. gold katika nywele zake

    ukiacha kuwa neymar ni mchezaji aliyetengeneza pesa nyingi sana katika soka lakini ametengeza pesa nyingi pia katika Endorsement za brands Neymar amekuwa balozi wa makampuni makubwa Duniani,
    Neymar amewahi kuwa balozi wa kampuni kubwa za vifaa vya michezo Kama NiKe, Jordan na kwa sasa anafanya kazi na Puma,
    ukiachana na endorsement za makampuni ya vifaa vya michezo Neymar pia amefanya kazi na anaendelea kufanya kazi na Brands nyingine nyingi tu tofauti kama Beats Electronics, EA Games, Gillette, MasterCard. McDonald’s, Red Bull, na REPLAY JEANS, BLAZE BET nk. ukiacha kufanya kazi na brands mbali mbali Neymar ana brand yake ya mavaziana iitwayo NJr ambayo inauzwa kwa mashabiki. kwahiyo neymar kwake fashion ni maisha.

    Ukizungumzia watu wanaozipenda familia zao, basi neymar anaupendo mkubwa sana kwa familia yake Ana uhusiano wa karibu sana na baba yake mzazi, Neymar Santos Sr. (ambaye pia ni meneja wake), mama yake Nadine, na dada yake Rafaella. Rafaella, ambaye ni mwanamuziki na blogerr maarufu brazil. mara nyingi Neymar kila mwisho wa mwaka hufanya mtoko wa kifamilia.
    Neymar ni babaa watoto watatu kila mtoto ma mama yake, Mwanawe wa kwanza ni wa kiume aitwae Davi Lucca (aliyezaliwa 2011), aliyempata kwa aliyekuwa girlfriend wake Carolina Dantas, mwanae wa pili ni wa kike anaitwa Mavie mama yake anaitwa Bruna Biancardi, na wa mwisho ni wa kike aitwae Hellen alimpata mwaka wa jana 2024. kwa Amanda Kimberlly, mwaka huu amerudiana tenah na mama wa mtoto wake wa pili Bruna biancardi na wanatarajia kupata mtoto mwingine hivi karibuni maana bdada huyo ni mjamzito kwa sasa. na wawili hao wako mbioni kufunga ndoa ya kanisani.

    pamoja na kuwa na mahusiano hio haimzuii Neymar kukutana na wanae hao wengine, amekuwa na utaratibu wa kukutana na watoto wake wote katika baadhi ya mechi, Neymar hupenda kutumia wakati mwingi na mtoto wake,
    mtoto wake wa kwanza Davi Lucca anapenda kucheza mpira na anasoma Barcelona’s Escola school, shule ya ball ya barcelona ambapo watoto wakitoka hapo wanajiunga na academy kuu ya Barcelona La masia academy,

    Neymar ni mtu wa watu neymar yupo miongoni mwa wale wachezaji wenye 0 hatters, yaani ukimchukia neymar basi umeuchukia na mpira wenyewe, neymar ni rafiki wa watu wengi. mashuhuri, kama kina Lionel Messi na Kylian Mbappé, Vini jr , raphinha, Rodrygo, Suarez, Lamine yamal lakini pia hana baya pia Cr7 ni mtu wa watu huyu mwamba.

    Watu wengi husema kipindi cha ujana wake aliponda sana raha, umaarufu ulimuendesha kwa kiasi, na wengine hufika mbali na kusema kuwa huenda hata injury alizokuwa akizipata kwenye mpira ni sababu ya kula bata na kuwa mvuvi wa mazoezi,

    Neymar pia ni mpenzi wa muziki. Ameshiriki katika video za muziki za wasanii kama Sertanejo na Funk Brasileiro, na mara kadhaa hutembelea studio za music Alishiriki kwenye wimbo wa MC Kevinho, “Tudo Ok”, akionyesha uwezo wake wa kuimba na kucheza densi. Mara nyingi neymar amekuwa akiarikwa kwenye matukio makubwa ya mziki kama tuzo mbalimbali kama vile grammy katika miji kama Paris, Miami, au Rio dijeneiro.

    Neymar Aliwahi kukabiliana na kashfa za kukwepa kodi serikalini, mashtaka ya ubakaji (ambayo alikataa na kusitishwa mwaka 2021),

    Ukiachilia mbali, Ubishoo wake, Tatoos zake mwilini neymar ni mtu wa imani sana, pamoja na mali umaarufu aliokuwa nao lakini anaamini kuwa fedhe, dhahabu, umaarufu, maisha mazuri vyote hutoka kwa Mungu, kwahiyo anaikumbuka vyema nyumba ya ibada siyo tu wakati wa matatizo bali hata wakati wa raha, neymar toka utoto wake alipenda kwenda kanisani mpaka leo, Neymar ni muumini mzuri dini ya kikristo, neymar huamini katika yesu kristo hata alivyokuwa mdogo wakati akiitumikia academy ya santos alipenda kufunga kitambaa kichwani chenye maandishi ya 100% Jesus hata hivi karibuni alivyorejea kwa mara ya pili klabuni hapo wakati wa utambulisho wake alifunga kitambaa hicho cha 100% Jesus katika paji lake la uso, lakini pia alipokabidhiwa locker yake ya jezi aliweka kitabu kitakatifu cha biblia na alipiga goti na kufanya Dua katika Locker yake.

    Neymar ni mtoto wa kiBrazil aliyepambana kwa hali na mali kufanikiwa katika soka, neymar ni mtoto mwenye Familia yenye upendo, na mjasiriamali mwenye ndoto. Anaamini kuwa “maisha ni mchezo mzuri zaidi kuliko soka lenyewe.”* Asante kwa kunisikiliza dodosha comment yako hapo kwenye comment kama ulikuwa sambamba na mimi mwanzo mpaka mwisho, fanya kusubscribe kama bado hii hapa ni supa 12 ya dino television mi naitwa Dennis Dinomineta tukutane tenah panapo majariwa yake mwenyewezi Mungu.

  • Hello world!

    Welcome to WordPress. This is your first post. Edit or delete it, then start writing!